LOADING ...
Hicho Dr kigwangala anacho kinena ni kweli kabisaaa! don't wait to be treated the same as you treat them/ don't wait to be paid the happiness,love and prosperity that's you transfered to them.

Dr. Hamisi A. Kigwangalla

Nje ya Box ya leo itahusu kutoa na kujitoa. Niliwahi kusema hapa ‘Love is all about giving, not receiving!’ Leo napenda kusema kuwa ‘upendo zaidi ni kutoa na ama kujitolea’.

Wanazuoni wa kiislamu husema kwamba ‘katika funguo za mafanikio yako basi kutoa na kujitolea ni ya uhakika zaidi na Mungu anaipenda zaidi’.

Hebu jiulize atajisikiaje mjane ukamtembelea mwisho wa mwezi na hana pesa ya kulipa pango na yu mbioni kufukuzwa kwenye nyumba, nawe ukamlipia? Ama mtu ambaye amekata tamaa ya maisha, hana hakika ya kesho yake nawe ukamrejeshea matumaini, furaha na utulivu wa moyo?

Njia nyingine ya kufungua mafanikio yako ni kupambana kwa ajili ya wengine; rafiki, ndugu, jamaa, jamii ama nchi yako. Kuna faida kubwa sana pale mshkaji ana issue yake nawe ukakimbia huku na kule kumsaidia.

Si tu Mungu anafurahia tunaposhikamana na kusaidiana lakini angalia ‘deni’ utakalompa jamaa kwa kwenda mbio maili kadhaa zaidi ya inavyotarajiwa mpaka naye akafanikiwa! #HK #NjeYaBox

5 likes / 0 comments